65. Allaah hakuna maneno na matendo isipokuwa yaliyo mazuri

Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

الصلوات

maana yake ni du´aa zote na imesemekana kuwa maana yake ni zile swalah tano.

الطيبات

Allaah ni Mzuri na wala hayakubali maneno na vitendo isipokuwa mazuri tu.

MAELEZO

Allaah ndiye Mwenye kuabudiwa kwa vile vipindi vitano vya swalah. Kwa sababu Yeye ndiye Mwenye kuabudiwa kwa haki.

Matendo na maneno yote mazuri ni kwa ajili ya Allaah. Allaah ni Mzuri na wala hayakubali maneno na vitendo isipokuwa mazuri tu. Muslim amepokea katika “as-Swahiyh” yake kupitia kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye ameismulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Enyi watu! Hakika Allaah ni Mzuri na wala hakubali isipokuwa kilicho kizuri.”[1]

Hakika Yeye (Subhaanah) ni Mzuri na wala hakuna maneno na matendo isipokuwa yaliyo mazuri. Kwa msemo mwingine yaliyofanywa kwa ajili Yake pekee na yenye kuafikiana na Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayi sallam).

[1] Muslim (1015).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 96-97
  • Imechapishwa: 28/06/2022