65. al-Qummiy upotoshaji wake wa tano wa Aal ´Imraan

al-Qummiy amesema pindi alipokuwa akifasiri Aayah:

وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّـهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا

“Na shikamaneni kwa kamba ya Allaah nyote pamoja na wala msifarikiane!”[1]

“Upwekeshaji na uongozi. Abul-Jaaruud amepokea kupitia kwa Abu Ja´far aliyesema: “Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) alijua kuwa watatofautiana baada ya Mtume wao. Ndio maana Akawakataza kufarikiana na akawaamrisha kukusanyika juu ya uongozi wa familia ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”[2]

Kushikamana na kamba ya Allaah ni Qur-aan na Sunnah na I´tiqaad, hukumu, mu´amala na Shari´ah zengine zilizomo ndani yake. Mazanadiki hawa wanawakimbiza watu kutoka katika ´Aqiydah na matendo haya na kuwavuta katika ´Aqiydah ya Raafidhwah ambayo inaipiga vita Qur-aan, Sunnah, waislamu na khaswa ´Aliy na familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

´Aliy na familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wameamrishwa kushikamana na Qur-aan na Sunnah na wamekatazwa kufarikiana. Kile chenye kufanya kazi kwa waislamu kinawagusa wao pia. Wao ni watu wa kawaida ambao wanapatia na kukosea. Yale wanayoyasema ambayo yanaafikiana na Qur-aan na Sunnah, ni wajibu kuyakubali, na yale wanayokosea haijuzu kuyakubali. Yale yenye kufanya kazi kwa wanachuoni wa waislamu katika Maswahabah, Taabi´uun, waliokuja baada ya Taabi´uun na waliokuja baada yao, kinafanya kazi vilevile kwao pia; maneno ya kila mmoja yanakubaliwa na kukataliwa.

[1] 03:103

[2] Tafsiyr al-Qummiy (1/108).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 103
  • Imechapishwa: 03/04/2017