64. Uwajibu wa kutulizana kati ya Sujuud mbili


Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiketi kwa kutulizana mpaka kila mfupa unarudi mahala pake[1]. Alimwamrisha yule mwanamume aliyeswali kimakosa kufanya hivo na kumwambia:

“Hakuna swalah ya yeyote inayotimia mpaka afanye hivo.”[2]

Alikuwa anairefusha mpaka inakuwa ndefu kukaribia Sujuud yake[3]. Wakati mwingine akirefusha mpaka watu wakaanza kufikiria kuwa amesahau[4].

[1] Abu Daawuud na al-Bayhaqiy kwa mlolongo wa wapokezi Swahiyh.

[2] Abu Daawuud na al-Haakim aliyeisahihisha na adh-Dhahabiy akaafikiana naye.

[3] al-Bukhaariy na Muslim.

[4] al-Bukhaariy na Muslim. Ibn-ul-Qayyim amesema:

“Sunnah hii iliachwa na watu wengi tokea wakati wa karne ya Maswahabah. Kuhusu yule mwenye kuiacha Sunnah iongoze na asimjali yule mwenye kwenda kinyume nayo, mtu huyu hajali yale yanayokwenda kinyume na mwongozo huu.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 132-133
  • Imechapishwa: 07/08/2017