64. Mwenye kujilipua na kujiua haamini Qadhwaa´ na Qadar


Leo hii mnasikia sana yale yanayoitwa “kujilipua/kujiua” na kwamba ni jambo limeenea kati ya watu wenye dini zengine. Sababu yake ni nini? Sababu yake ni kutoamini Qadhwaa´ na Qadar. Pindi mmoja wao anapohisi dhiki anajilipua. Kwa sababu haamini Qadhwaa na Qadar. Hasemi kuwa ni jambo alilokadiriwa na kuandikiwa na akaamini kuwa faraja iko karibu na akamdhania Allaah vyema:

فَإِنَّ مَعَ الْعُسْرِ يُسْرًا

“Hakika pamoja na kila gumu kuna mepesi.” (94:05)

أَلَا إِنَّ نَصْرَ اللَّـهِ قَرِيبٌ

“Tanabahi! Hakika nusura ya Allaah iko karibu.” (02:214)

Ambaye anajilipua na kujiua haamini Qadhwaa´ na Qadar. Hawezi kustahamili matatizo na misiba.