64. Makatazo ya muislamu kuwasifu na kuwasema kwa uzuri makafiri


10- Miongoni mwa mambo yanayopelekea katika kuwakufurisha washirikina na makafiri ni kutowatapa na kuwasifu. Kwa sababu Allaah amewasema vibaya. Isitoshe wao ni maadui wa Allaah na ni maadui wa Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Vipi basi utawasifu? Kwa sababu wapo baadhi ya watu wanaosema kuwa ni waaminifu, wanatangamana vizuri na sifa nyenginezo. Upande mwingine anawaponda waislamu na kusema kwamba waislamu wana khiyana, ghushi na mengineyo. Waislamu, japokuwa watakuwa na maasi kama ghushi, wao ni wabora katika walio ardhini. Lakini makafiri wao ni maadui wa Allaah na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hata kama watakuwa na baadhi ya sifa nzuri ambazo wanazitumia kwa ajili ya dunia yao. Haijuzu kuwasifu wakati Allaah (Jalla wa ´Alaa) amewasema kwa ubaya. Kinyume chake ni wajibu kwa muislamu kuwasema kwa ubaya kwa ajili ya kumkufuru kwao Allaah (´Azza wa Jall).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 92
  • Imechapishwa: 21/10/2018