64. Hakutikisiki kitu isipokuwa kwa msaada wa Allaah


Abu Muhammad ´Abdullaah bin Abiy Zayd al-Qayrawaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

Hapana shaka kwamba Yeye ndiye Mola wa waja na ndiye Mola wa matendo yao ambaye amewakadiria kutikisika kwao na muda wao wa kueshi.

MAELEZO

Allaah ndiye Mola wa waja. Yeye ndiye anawamiliki na kuwaendesha, Anawalea na kuwatunza kwa neema Zake. Yeye ndiye ambaye anazilea nyoyo zao kwa Wahy na miili yao kwa ruzuku. Yeye vilevile ndiye Mola wa matendo yao. Amesema (Ta´ala):

وَاللَّـهُ خَلَقَكُمْ وَمَا تَعْمَلُونَ

“… ilihali Allaah amekuumbeni pamoja na vile mnayoyafanya.”[1]

Amekuumbeni na akaumba yale mnayoyafanya. Hakuna yeyote ambaye anatenda kivyake au akaumba pasi na Allaah. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ndiye Mwenye kuumba. Kiumbe haumbi hata matendo yake mwenyewe. Yeye ndiye anawapangia kutikisika kwao na muda wao wa kueshi:

وَمَا تَحْمِلُ مِنْ أُنثَىٰ وَلَا تَضَعُ إِلَّا بِعِلْمِهِ ۚ وَمَا يُعَمَّرُ مِن مُّعَمَّرٍ وَلَا يُنقَصُ مِنْ عُمُرِهِ إِلَّا فِي كِتَابٍ ۚ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ

“Mwanamke yeyote habebi mimba na wala hazai isipokuwa kwa ujuzi Wake na hapewi umri mrefu yeyote yule mwenye umri mrefu na wala hapunguziwi katika umri wake isipokuwa yamo kitabuni. Hakika hayo kwa Allaah ni mepesi.”[2]

[1] 37:96

[2] 35:11

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 50
  • Imechapishwa: 09/08/2021