Kuna aina nne za eda:

Ya kwanza: Eda ya mjamzito. Muda wake ni kwa kule kuzaa mimba. Ni mamoja ameachwa talaka tatu au chini ya tatu ambapo anaweza kurejelewa, katika uhai wake au mume akafariki. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَاللَّائِي يَئِسْنَ مِنَ الْمَحِيضِ مِن نِّسَائِكُمْ إِنِ ارْتَبْتُمْ فَعِدَّتُهُنَّ ثَلَاثَةُ أَشْهُرٍ وَاللَّائِي لَمْ يَحِضْنَ ۚ وَأُولَاتُ الْأَحْمَالِ أَجَلُهُنَّ أَن يَضَعْنَ حَمْلَهُنَّ

“Wale wanawake wanaokoma hedhi miongoni mwa wanawake wenu, mkiwa mna shaka, basi eda yao ni miezi mitatu, pamoja na wale wanawake wasiopata hedhi. Na wenye mimba muda wao [wa eda] watakapozaa mimba zao.”[1]

Ya pili: Eda ya mwenye kuachwa ambaye hupata hedhi. Anatakiwa kupata hedhi tatu. Amesema (Ta´ala):

وَالْمُطَلَّقَاتُ يَتَرَبَّصْنَ بِأَنفُسِهِنَّ ثَلَاثَةَ قُرُوءٍ

“Wanawake waliotalikiwa wabakie kungojea zipite hedhi  [au twahara] tatu.”[2]

Bi maana hedhi tatu.

Ya tatu: Ambaye hapati hedhi. Wanawake hawa wamegawanyika aina mbili:

1 – Mdogo ambaye hajaanza kupata hedhi.

2 – Mkubwa ambaye hapati hedhi na amekwishakata tamaa ya kupata hedhi. Allaah (Subhaanah) amebainisha eda ya aina mbili za wanawake hawa pale aliposema:

وَاللَّائِي يَئِسْنَ مِنَ الْمَحِيضِ مِن نِّسَائِكُمْ إِنِ ارْتَبْتُمْ فَعِدَّتُهُنَّ ثَلَاثَةُ أَشْهُرٍ وَاللَّائِي لَمْ يَحِضْنَ

“Na wale wanawake wanaokoma hedhi miongoni mwa wanawake wenu, mkiwa mna shaka, basi eda yao ni miezi mitatu, pamoja na wale wanawake wasiopata hedhi.”[3]

Bi maana yeye pia ndivo ilivyo eda yake.

Ya nne: Ambaye amefiliwa na mumewe. Eda yake imebainishwa pale aliposema:

وَالَّذِينَ يُتَوَفَّوْنَ مِنكُمْ وَيَذَرُونَ أَزْوَاجًا يَتَرَبَّصْنَ بِأَنفُسِهِنَّ أَرْبَعَةَ أَشْهُرٍ وَعَشْرًا

“Na wale wanaofishwa miongoni mwenu na wakaacha wake, hao wake wangojee peke yao [eda ya] miezi minne na siku kumi.”[4]

Hii inamkusanya mwanamke ambaye ameingiliwa, ambaye hakuingiliwa, mdogo, mkubwa na wala haingii mjamzito ambaye ametoka kwa maneno Yake:

وَأُولَاتُ الْأَحْمَالِ أَجَلُهُنَّ أَن يَضَعْنَ حَمْلَهُنَّ

“Na wenye mimba muda wao [wa eda] watakapozaa mimba zao.”

Haya ni kutoka kwenye “al-Hadyi an-Nabawiy”[5] ya Ibn-ul-Qayyim katika chapa iliyohakikiwa.

[1] 65:04

[2] 02:228

[3] 65:04

[4] 02:234

[5] (05/594-595).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tanbiyhaat, uk. 111-112
  • Imechapishwa: 26/11/2019