63. Yanayomlazimu mwanamke wakati unapoisha mkataba wa ndoa yake

Kuna aina mbili za mume na mke kutengana:

1 – Wakatengana wakiwa hai.

2 – Wakatengana kwa kifo.

Katika hali zote mbili ni lazima kwa mwanamke kukaa eda. Ni kungojea muda uliowekwa katika Shari´ah. Hekima yake ni ukuta wa kumalizika hiyo ndoa baada ya kumalizika ndoa hiyo na kutakasika ule mfuko wa uzazi kutokana na mimba ili asije kumjamii yule asiyefarikiana naye. Matokeo yake kukatokea utatizi na kupoteza nasabu. Pia ndani yake kuna kuheshimu ndoa ya yule mume aliyetangulia, kuheshimu haki ya mume aliyemwacha na kudhihirisha kuathirika kwa kumwacha.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tanbiyhaat, uk. 110-111
  • Imechapishwa: 26/11/2019