63. Nguzo ya kumi na mbili mpaka ya kumi na nne

12 – Nguzo ya kumi na mbili: Kukaa katika Tashahhud hiyo. Kwa msemo mwingine ni kwamba anatakiwa kuisoma Tashahhud hiyo hali ya kuwa ameketi chini na si mwenye kusimama.

13 – Nguzo ya kumi na tatu: Kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Tashahhud ya mwisho.

Kuna tofauti kati ya wanazuoni. Imesemekana kwamba ni nguzo. Pia imesemekana vilevile kwamba ni wajibu. Yako maoni vilevile yanayosema kuwa imependekezwa[1]. Maoni yaliyo karibu zaidi na usawa ni kwamba ni wajibu.

14 – Nguzo ya kumi na nne: Tasliym mbili kwa yeye kusema:

السلام عليكم ورحمة الله

“Amani na baraka za Allaah ziwe juu yenu.”

Atasema hivo upande wa kuliani na wa upande wa kushotoni.

Mpaka hapa zimetimia nguzo kumi na nne.

[1] Tazama ”Ikhtilaaf-ul-A-immat-il-´Ulamaa” (01/120-121) ya Ibn Abiy Hubayrah, ”al-Mughniy” (01/367) na ”al-Majmuu´” (03/430).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 93-94
  • Imechapishwa: 24/06/2022