63. Makatazo ya kuwaacha makafiri wakamakinika na kutanua katika kisiwa cha kiarabu


9- Miongoani mwa mambo yanayopelekea katika kuwakufurisha washirikina na makafiri ni kwamba ni lazima kwa mtawala kuwaondosha kutoka katika kisiwa cha kiarabu[1]. Kwa sababu kisiwa cha kiarabu ndio chemchem ya ujumbe na ndio chemchem ya Da´wah. Kwa hivyo haijuzu kubaki dini nyingine yoyote zaidi ya Uislamu. Wasiachwe wakaishi katika kisiwa cha kiarabu kwa njia ya umilele. Ama kuwaachia wasafiri kwa ajili ya biashara na safari zengine mfano wa hayo, haina neno. Lililokatazwa ni kuwaacha wakaishi na kumiliki katika kisiwa cha kiarabu. Kwa sababu Mtume (Swallah Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema wakati wa kufa kwake:

“Watoeni mayahudi na manaswara katika kisawa cha kiarabu.”[2]

Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Kusibaki katika kisiwa cha kiarabu dini mbili.”[3]

´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) akatekeleza wasia huu wakati wa ukhalifa wake.  Akawatoa mayahudi na manaswara katika kisiwa cha kiarabu.

Kuhusu wakiingia na kutaka kuishi kwa muda maalum kwa sababu ya jambo muhimu miongoni mwa mambo muhimu, kusafiri katika kisiwa cha kiarabu, basi haitotakikana kuwaacha wakadhihirisha alama zao; wasiachwe wakajenga makanisa katika miji ya waislamu. Isipokuwa linatakiwa kufupizwa jambo lao kati yao katika zile sehemu wanazoishi kwa muda maalum. Haitakikani wakaachwa wakadhihirisha ukafiri wao katika miji ya waislamu kama kwa mfano kusimika misalaba na kupiga kengele. Hili si jambo linalowahusu mayahudi na manaswara peke yao. Ni jambo linawahusu washirikina wote wakiwemo waabudu makaburi na wengineo. Hatawakiwi kuachwa wakajenga makaburi yao. Hawatakiwi kuachwa wakaijenga misikiti juu ya makaburi. Ni wajibu kwa mtawala wa waislamu kuyabomoa makaburi haya. Kila mshirikina asiachwe akadhihirisha shirki zake katika miji ya waislamu.

[1] Shaykh wetu amesema hali ya kuwa ni mwenye kuliwekea hili taaliki:

“Hii ni kazi maalum inayomuhusu mtawala wa waislamu. Haijuzu kwa yeyote kuwaondoa, kama wanavoonelea hii leo wajinga katika vijana na wale walioathirika na maoni ya Khawaarij. Matokeo yake wakawa wanawaua wale walioahidiwa usalama na waliopewa mkataba wa amani, wanalipua majengo ambayo hawa makafiri walioahidiwa usalama na waliopewa mkataba wa amani wanaishi ndani yake. Hivyo wakawa wanafanya usaliti dhimma ya waislamu na wanakhaini ahadi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kumuua aliyepewa mkataba basi hatonusa harufu ya Pepo.”

[2] al-Bukhaariy (3053), Muslim (163), Abu Daawuud (3029) na Ahmad (1691). Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy.

[3] Ameipokea at-Twabaraniy katika “al-Awsatw” (1066) kutoka kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) na wengineo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 90-92
  • Imechapishwa: 21/10/2018