63. Hakuna Muumbaji yeyote asipokuwa Allaah

Abu Muhammad ´Abdullaah bin Abiy Zayd al-Qayrawaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

Hakuna chochote isipokuwa kimeumbwa Naye.

MAELEZO

Hakuna chochote ambacho kimeumbwa na mwingine isipokuwa na Allaah. Kila kilichopo ulimwenguni kimeumbwa na Allaah. Amesema (Ta´ala):

اللَّـهُ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ ۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ وَكِيلٌ

”Allaah ni Muumbaji wa kila jambo, Naye juu ya kila jambo ni mdhamini.”[1]

هَـٰذَا خَلْقُ اللَّـهِ فَأَرُونِي مَاذَا خَلَقَ الَّذِينَ مِن دُونِهِ ۚ بَلِ الظَّالِمُونَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ

”Huu ni uumbaji wa Allaah, basi nionyesheni nini walichokiumba wasiokuwa Yeye. Bali madhalimu wamo katika upotevu wa wazi.”[2]

قُلْ أَرَأَيْتُم مَّا تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ أَرُونِي مَاذَا خَلَقُوا مِنَ الْأَرْضِ أَمْ لَهُمْ شِرْكٌ فِي السَّمَاوَاتِ ۖ ائْتُونِي بِكِتَابٍ مِّن قَبْلِ هَـٰذَا أَوْ أَثَارَةٍ مِّنْ عِلْمٍ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ

”Sema: ”Je, mnaonaje wale mnaowaomba badala ya Allaah! Nionyesheni nini wameumba katika ardhi au wana ushirika katika mbingu? Nileteeni Kitabu kabla ya hiki au alama yoyote iliobakia ya elimu mkiwa ni wakweli.”[3]

Thibitisha kwamba kitu fulani kimeumbwa na mtu fulani. Kitu kama hicho hawawezi kukithibitisha. Ni changamoto kutoka kwa Allaah (´Azza wa Jall). Changamoto inathibitisha kuwa vyote vilivyomo ulimwenguni vimeumbwa na Allaah. Allaah pekee ndiye Muumba na vyenginevyo vyote vimeumbwa. Amesema (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا النَّاسُ ضُرِبَ مَثَلٌ فَاسْتَمِعُوا لَهُ ۚ إِنَّ الَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ لَن يَخْلُقُوا ذُبَابًا وَلَوِ اجْتَمَعُوا لَهُ

“Enyi watu! Imepigwa mfano basi isikilizeni kwa makini! Hakika wale mnaowaomba badala ya Allaah hawawezi kuumba nzi japo wakijumuika kwa hilo.”[4]

[1] 39:62

[2] 31:11

[3] 46:4

[4] 22:73

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 50
  • Imechapishwa: 09/08/2021