63. al-Iq´aa’ kati ya Sujuud mbili

Wakati mwingine alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anaweza kuketi mtindo wa al-Iq´aa’ ambapo anakalia visigino vyake na vidole vyake[1].

[1] Muslim, Abu ´Awaanah, Abuush-Shaykh katika ”Maa rawaahu Abuuz-Zubayr ´an Jaabir” (104-106) na al-Bayhaqiy. Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesahau pindi alipotaja kikao cha Mtume  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) baina ya Sujuud mbili:

“Haikupokelewa ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliikaa kikao hichi kwa mtindo mwingine isipokuwa hichi tu.”

Ni vipi itakuwa sahihi ilihali al-Iq´aa’ imepokelewa kupitia Hadiyth ya Ibn ´Abbaas katika al-Bukhaariy, Abu Daawuud na at-Tirmidhiy aliyeisahihisha? Tazama “as-Swahiyhah” (383). Kadhalika Hadiyth hiyo imepokelewa na al-Bayhaqiy kwa mlolongo wa wapokezi mzuri kupitia kwa Ibn ´Umar ambayo imesahihishwa na Ibn Hajar. Abu Ishaaq al-Harbiy ameipokea katika “Ghariyb-ul-Hadiyth” (01/12/05) kutoka kwa Twaawuus ambaye anaonelea kuwa Ibn ´Umar na Ibn ´Abbaas walikaa mtindo wa al-Iq´aa’. Mlolongo wa wapokezi ni Swahiyh. Allaah amrehemu Imaam Maalik aliyesema: “Hakuna yeyote katika sisi isipokuwa maneno yake yanakubaliwa na kurudishwa isipokuwa huyu aliyemo ndani ya kaburi hili” na akaashiria kaburi la  Mtume  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Sunnah hii ilitendewa kazi na Maswahabah wengi, Taabi´uun na wengineo. Hata hivyo al-Iq´aa’ hii sio ile iliyokatazwa, kama itavyokuja huko katika Tashahhud.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 132
  • Imechapishwa: 07/08/2017