62. Uthibitisho ya kwamba shirki ya watu wa kale ni khafifu kuliko shirki ya watu wa zama zetu II

Atakayefahamu masuala haya ambayo Allaah ameyaweka wazi katika Kitabu Chake – nayo ni kwamba washirikina ambao Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwapiga vita walikuwa wakimuomba Allaah (Ta´ala) na wakiwaomba wengine katika raha, ama wakati mgumu na wa shida hawamuombi mwengine isipokuwa Allaah pekee hali ya kuwa hana mshirika na wanawasahau mabwana wao – umembainishia tofauti baina ya watu wa zama zetu na shirki ya watu wa mwanzo. Lakini ni nani ambaye moyo wake unayafahamu mambo haya ufahamu wa ndani kabisa? Allaah ndiye Mwenye kutakwa msaada.

MAELEZO

Anasema (Rahimahu Allaah):

Hatambui tofauti kati shirki ya watu wa kale na shirki ya watu waliokuja nyuma ya kwamba shirki ya watu waliokuja nyuma ni khatari na kubwa zaidi. Haya hayafahamiki na yeyote isipokuwa yule mwenye kuzifahamu Aayah za Qur-aan zinazoyatia hayo wazi. Asiyeona tofauti basi inatokamana na kufahamu kwake vibaya.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 93
  • Imechapishwa: 27/01/2017