62. Ni Sunnah kumuharakisha maiti


Swali 62: Je, imesuniwa kuharakisha jeneza[1]?

Jibu: Imesuniwa kuharakisha jeneza pasi na tabu.  Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Fanyeni haraka kumwandaa maiti. Akiwa ni mwema basi ni kheri mnazomtangulizia. Akiwa hayuko hivo ni shari mnayoitua kutoka shingo zenu.”[2]

Kuna maafikiano juu ya usahihi wake.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/180).

[2] al-Bukhaariy (1315) na Muslim (944).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 46
  • Imechapishwa: 26/12/2021