62. Makatazo ya kuwaacha makafiri wakaingia mji wa Makkah

8- Kutowaacha wakaingia Makkah Takatifu. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْمُشْرِكُونَ نَجَسٌ فَلَا يَقْرَبُوا الْمَسْجِدَ الْحَرَامَ بَعْدَ عَامِهِمْ هَـٰذَا ۚوَإِنْ خِفْتُمْ عَيْلَةً فَسَوْفَ يُغْنِيكُمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ إِن شَاءَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ حَكِيمٌ

”Enyi mlioamini!  Hakika washirikiana ni najisi. Hivyo basi wasikaribie al-Masjid al-Haraam baada ya mwaka wao huu. Mkikhofu umasikini basi Allaah atakutajirisheni kutokana na fadhila Zake akitaka.  Hakika Allaah ni Mjuzi, Mwenye hekima.” (at-Tawbah 09:28)

Wakati Aayah hii ilipoteremka Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamtuma ´Aliy awatangazie katika msimu wa hajj ya kwamba baada ya mwaka huu haifai kwa mshirikina yeyote kuhiji na wala asitufu yeyote katika Nyumba akiwa uchi[1]. Tokea wakati huo wakazuiwa kuingia Haram. Vilevile wanatakiwa kuendelea kuzuiwa mpaka Qiyaamah kitaposimama. Amesema (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْمُشْرِكُونَ نَجَسٌ فَلَا يَقْرَبُوا الْمَسْجِدَ الْحَرَامَ

”Enyi mlioamini!  Hakika washirikiana ni najisi. Hivyo basi wasikaribie al-Masjid al-Haraam.”

Makusudio ya kuwazuia haina maana kwamba ni kuwazuia kuingia msikitini peke yake. Bali inatakiwa kuwazuia kuingia Makkah yote:

فَلَا يَقْرَبُوا الْمَسْجِدَ الْحَرَامَ بَعْدَ عَامِهِمْ هَـٰذَا

“Hivyo basi wasikaribie al-Masjid al-Haraam baada ya mwaka wao huu.”


[1]
Ameipokea al-Bukhaariy (369) na Muslim (1347) kupitia kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 89-90
  • Imechapishwa: 21/10/2018