61. Uthibitisho ya kwamba shirki ya watu wa kale ni khafifu kuliko shirki ya watu wa zama zetu

Ukishajua kile wanachoita washirikina katika zama zetu hizi “Itikadi” ndio shirki iliyoteremka katika Qur-aan juu yake na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawapiga vita watu kwa ajili yayo, basi ujue kuwa shirki ya watu wa mwanzo ni khafifu kuliko shirki ya watu wa zama zetu kwa mambo mawili.

La kwanza: Watu wa mwanzo walikuwa hawashirikishi na wala hawawaombi Malaika, mawalii na masanamu pamoja na Allaah isipokuwa wakati wa raha. Ama wakati wa shida, walikuwa ni wenye kumtakasia Allaah dini. Kama alivyosema (Ta´ala):

وَإِذَا مَسَّكُمُ الضُّرُّ فِي الْبَحْرِ ضَلَّ مَن تَدْعُونَ إِلَّا إِيَّاهُ ۖ فَلَمَّا نَجَّاكُمْ إِلَى الْبَرِّ أَعْرَضْتُمْ ۚ وَكَانَ الْإِنسَانُ كَفُورًا

”Na inapokuguseni dhara baharini hupotea wale mnaowaomba isipokuwa [mnamwita] Yeye pekee. Lakini Anapokuokoeni kwa kuwafikisha nchi kavu, mnakengeuka; na binaadamu daima ni mwingi wa kukanusha.” (al-Israa´ 17 : 67)

Na Kauli Yake (Ta´ala):

قُلْ أَرَأَيْتَكُمْ إِنْ أَتَاكُمْ عَذَابُ اللَّـهِ أَوْ أَتَتْكُمُ السَّاعَةُ أَغَيْرَ اللَّـهِ تَدْعُونَ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ بَلْ إِيَّاهُ تَدْعُونَ فَيَكْشِفُ مَا تَدْعُونَ إِلَيْهِ إِن شَاءَ وَتَنسَوْنَ مَا تُشْرِكُونَ

”Sema: “Je mnaonaje ikikufikieni adhabu ya Allaah au ikakufikieni Saa; je, mtamwomba asiyekuwa Allaah mkiwa ni wakweli?” Bali Yeye pekee ndiye mtakayemwomba, kisha atakuondoleeni yale mliyomwomba Akitaka, na mtasahau yale mnayoyashirikisha pamoja Naye.”” (al-An´aam 06 : 40-41)

Na Kauli Yake (Ta´ala):

وَإِذَا مَسَّ الْإِنسَانَ ضُرٌّ دَعَا رَبَّهُ مُنِيبًا إِلَيْهِ ثُمَّ إِذَا خَوَّلَهُ نِعْمَةً مِّنْهُ نَسِيَ مَا كَانَ يَدْعُو إِلَيْهِ مِن قَبْلُ وَجَعَلَ لِلَّـهِ أَندَادًا لِّيُضِلَّ عَن سَبِيلِهِ ۚ قُلْ تَمَتَّعْ بِكُفْرِكَ قَلِيلًا ۖ إِنَّكَ مِنْ أَصْحَابِ النَّارِ

”Na inapomgusa binaadamu dhara, humwomba Mola wake akirudiarudia Kwake hali ya kutubia, kisha Akimtunukia neema kutoka Kwake husahau yale aliyokuwa akimwomba kabla na kumfanyia Allaah washirika ili apotee na Njia Yake. Sema: “Starehe kwa kufuru yako kidogo tu. Hakika wewe ni miongoni mwa watu wa motoni!”” (az-Zumar 39 : 08)

Na Kauli Yake (Ta´ala):

وَإِذَا غَشِيَهُم مَّوْجٌ كَالظُّلَلِ دَعَوُا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ

”Na yanapowafunika mawimbi kama vivuli, humwomba Allaah hali ya kumtakasia Yeye dini.” (Luqmaan 31 : 32)

MAELEZO

Shaykh (Rahimahu Allaah) anasema:

Ukitambua kutokamana na yale yaliyotangulia kwamba hakuna tofauti kati ya shirki ya wa wale watu wa kipindi cha kishirikina ambao Qur-aan imeteremka juu yao na ambao walipigwa vita na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah wake na shirki ya watu hawa ambao wanajinasibisha na Uislamu katika waabudu makaburi, watu wa vijia vilivyopinda vya Suufiyyah na mfano wao. Hakuna tofauti kati ya shirki ya watu hawa na hawa. Tofauti iliyopo tu ni katika jina kwa kuwa wao wanaita “I´tiqaad” peke yake.

Tambua kuwa shirki ya watu hawa waliokuja nyuma wanaojinasibisha na Uislamu ni khatari na mbaya zaidi kuliko shirki ya wale watu wa kale wa kipindi cha kishirikina. Hilo linatambulika kwa njia mbili:

Ya kwanza: Shirki ya watu wa kale walikuwa wakishirikisha katika kipindi cha raha. Ama kipindi cha matatizo walikuwa wakiacha shirki na badala yake wanamtakasia du´aa Allaah kwa kutambua kwao kwamba hakuna anayeokoa kutokamana na matatizo isipokuwa Allaah (Subhaanah). Allaah ametaja hayo kuhusu wao katika Aayah zilizotajwa na Shaykh na wengineo.

Kuhusu washirikina hawa wanaojinasibisha na Uislamu shirki zao zinakuwa daima katika kipindi cha raha na cha shida. Bali ni kwamba shirki zao katika kipindi cha shida zinakuwa ni nyingi kuliko katika kipindi cha raha. Kwa vile wanapotumbukia katika hali ya khatari na shida basi wananyanyua sauti zao kwa shirki na kumuomba asiyekuwa Allaah. Namna hii ndivyo ilivyo tofauti kati ya washirikina wa mwanzo na washirikina wa wakati wetu huu.

Ya pili: Itakuja huko mbele.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 91-92
  • Imechapishwa: 25/01/2017