61. Mwanamke amekatazwa kusindikiza jeneza makaburini II


Swali 61: Hadiyth ya ´Umm ´Atwiyyah:

“Tumekatazwa kufuata jeneza na wala hatukutiliwa mkazo.”[1]

Ifahamike vipi?

Jibu: Inafahamika kwamba kwa mtazamo wake makatazo hayakutiliwa mkazo. Kimsingi ni kwamba makatazo yanapelekea katika uharamu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yale niliyokukatazeni basi jiepusheni nayo na yale niliyokuamrisheni basi yaendeeni kiasi muwezavyo.”[2]

Kuna maafikiano juu ya usahihi wake.

Hiyo inajulisha juu ya uharamu wa wanawake kuyasindikiza majeneza kwenda makaburini. Kuhusu kumswalia maiti ni jambo limewekwa katika Shari´ah kwao kama wanamme.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/178).

[2] Ahmad (7288) na Muslim (1337).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 45-46
  • Imechapishwa: 26/12/2021