61. Makatazo ya kuwaacha makafiri wakajitanua


7- Wasitangulizwe katika vikao na wala wasifunguliwe njia. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

 “Mtapokutana nao njiani basi wasogezeni upande wenye dhiki zaidi.”[1]

Hawakatazwi kupita lakini hata hivyo hawafunguliwi njia kupita kama wanavyofunguliwa waislamu, isipokuwa waachwe wapite katika njia za pembeni. Yote haya ni kwa ajili ya kuwatweza kwa sababu Allaah Mwenyewe kawatweza.

[1] Ameipokea al-Bukhaariy katika “al-Aadab al-Mufrad” (1103), Muslim (2167), at-Tirmidhiy (1602 na Abu Daawuud (5205) kupitia kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh). Vilevile imepokelewa na Ahmad (7567). at-Tirmidhiy amesema:

“Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 89
  • Imechapishwa: 16/10/2018