Jabriyyah hawatekelezi maneno haya waliyosema katika mambo yote. Lau kutakuwepo mtu ambaye atawafanyia mashambulizi, ni mamoja iwe kwa kumpiga au kumuua mmoja wao, hawatoomba kulipiza kisasi? Kwa nini waombe kufanya hivo ilihali wao wanasema kuwa ametenzwa nguvu na hakufanya kwa khiyari yake? Huku ni kujigonga.

Jengine ni kuwa wao wanatafuta riziki na wanaoa. Iwapo kweli wametenzwa nguvu, kama wanavyodai, ni kwa nini basi wanafanya mambo haya na wanatafuta kupatikana kwa mambo yasiyokuwepo? Wao hawatendei kazi ´Aqiydah hii chafu katika uhalisia wa maisha. Kwa ajili hiyo wanaomba kulipiza kisasi, wanaoa na wanatafuta riziki. Haya ni maneno batili. Hii ndio natija ya kutegemea fikira, akili mbovu, maneno au maoni ya watu pasi na kurejea katika Qur-aan na Sunnah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Mandhuumat-ul-Haaiyyah fiy ´Aqiydati Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 146
  • Imechapishwa: 11/01/2024