61. al-Qummiy upotoshaji wake wa nne wa Aal ´Imraan

al-Qummiy amesema:

“Kisha Allaah (´Azza wa Jall) akataja wale wenye kuvunja ahadi ya Allaah juu ya kiongozi wa waumini na wakakufuru baada ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kusema:

كَيْفَ يَهْدِي اللَّـهُ قَوْمًا كَفَرُوا بَعْدَ إِيمَانِهِمْ وَشَهِدُوا أَنَّ الرَّسُولَ حَقٌّ وَجَاءَهُمُ الْبَيِّنَاتُ ۚ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ أُولَـٰئِكَ جَزَاؤُهُمْ أَنَّ عَلَيْهِمْ لَعْنَةَ اللَّـهِ وَالْمَلَائِكَةِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ خَالِدِينَ فِيهَا لَا يُخَفَّفُ عَنْهُمُ الْعَذَابُ وَلَا هُمْ يُنظَرُونَ إِلَّا الَّذِينَ تَابُوا مِن بَعْدِ ذَٰلِكَ وَأَصْلَحُوا فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بَعْدَ إِيمَانِهِمْ ثُمَّ ازْدَادُوا كُفْرًا لَّن تُقْبَلَ تَوْبَتُهُمْ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الضَّالُّونَ إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَمَاتُوا وَهُمْ كُفَّارٌ فَلَن يُقْبَلَ مِنْ أَحَدِهِم مِّلْءُ الْأَرْضِ ذَهَبًا وَلَوِ افْتَدَىٰ بِهِ ۗ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ وَمَا لَهُم مِّن نَّاصِرِينَ

“Ni vipi Allaah atawaongoza watu waliokufuru baada ya kuamini kwao na wakashuhudia kwamba Mtume ni haki na zikawajia hoja bainifu? [Sivyo,] Allaah hawaongozi watu madhalimu. Hao malipo yao ni kwamba juu yao ipo laana ya Allaah na ya Malaika na watu wote. Wenye kudumu humo hawatopunguziwa adhabu wala hawatopewa muda wa kuakhirishwa adhabu. Isipokuwa wale waliotubu baada ya hayo na wakatengemaa [hao hawatoadhibiwa] – Allaah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu. Hakika wale waliokufuru baada ya kuamini kwao kisha wakazidi kukufuru – tawbah yao haitokubaliwa; [hapana,] na hao ndio waliopotoka kabisa. Hakika wale waliokufuru na wakafa nao wakiwa makafiri, basi haitakubaliwa kutoka kwa mmoja wao [fidia ya] dhahabu ya kujaza dunia nzima lau wakitaka kujikombolea nayo. Hao watapata adhabu iumizayo na hawatopata mwenye kuwanusuru.”[1]

Aayah zote hizi ni kuhusu wale maadui wa familia ya Muhammad. Kisha akasema:

لَن تَنَالُوا الْبِرَّ حَتَّىٰ تُنفِقُوا مِمَّا تُحِبُّونَ ۚ وَمَا تُنفِقُوا مِن شَيْءٍ فَإِنَّ اللَّـهَ بِهِ عَلِيمٌ

“Hamtoweza kuufikia wema mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda na hakuna chochote mnachokitoa isipokuwa hakika Allaah kwacho ni mjuzi.”[2]

Bi maana hamtopewa thawabu yoyote mpaka mrudishe haki ya familia ya Muhammad ya khumusi, ngawira na fai.”[3]

Tazama namna ambavyo maadui wa Allaah wanazikengeusha Aayah zilizoteremshwa kwa wanafiki waliokufuru wakati wa uhai wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) baada ya wao kujiwa na hoja bainifu. Humo wanakemewa na kutishwa wanafiki hawa waliomkufuru Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Uislamu wote. Anazikengeusha Aayah kwa kitu kisichokuwepo kabisa na kisichopo katika Qur-aan na Sunnah. Si jengine isipokuwa tu ni uzushi uongo wa Ibn Sabaa´ na wafuasi wake mazanadiki wanapozipachika Aayah juu ya Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kuwatuhumu kuritadi, kutaka ionekane kwamba laana ya Allaah, Malaika Wake na watu wote iko juu yao, kuwahukumu kudumu Motoni milele na kadhalika.

Tazama jinsi anavyopotosha maana ya maneno ya Allaah (Ta´ala):

لَن تَنَالُوا الْبِرَّ حَتَّىٰ تُنفِقُوا مِمَّا تُحِبُّونَ ۚ وَمَا تُنفِقُوا مِن شَيْءٍ فَإِنَّ اللَّـهَ بِهِ عَلِيمٌ

“Hamtoweza kuufikia wema mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda na hakuna chochote mnachokitoa isipokuwa hakika Allaah kwacho ni mjuzi.”[4]

kwenda katika ´Aqiydah yake potofu katika fai, khumusi na ngawira. Ni kwa nini anafanya hivo? Kwa sababu viongozi wa Raafidhwah na mazanadiki wanapokonya pesa kutoka kwa wafuasi wao wapumbavu kwa kutumia jina la familia ya Muhammad na kwa kutumia jina la faida, khumusi na ngawira. Yote haya ni katika matunda ya Jihaad katika njia ya Allaah na waislamu wanajua namna vinavyotakiwa kutumiwa. Lakini hata hivyo viongozi wa Raafidhwah na mazanadiki wamejifaradhishia khumusi na wanafanya hivo kwa kutumia jina la familia ya Muhammad pasi na Jihaad. Bali wao hawaonelei kuwepo kwa Jihaad mpaka al-Mahdiy wao asiyekuwepo na wa uongo atokee. Ni vipi atatokea?

[1] 03:86-91

[2] 03:91

[3] Tafsiyr al-Qummiy (1/107).

[4] 03:91

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 99
  • Imechapishwa: 03/04/2017