61. Afanye nini kama mke anamchukia mume na hataki kubaki naye?

Allaah (Ta´ala) amesema:

فَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا يُقِيمَا حُدُودَ اللَّـهِ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا فِيمَا افْتَدَتْ بِهِ

“Mtakapochelea kuwa wote wawili hawatoweza kusimamisha mipaka ya Allaah, basi hakuna neno juu yao katika ambacho amejikombolea kwacho.”[1]

Haafidhw Ibn Kathiyr amesema katika “Tafsiyr” yake:

“Mume na mke wakigombana na mke asitekeleze haki za mume, akamchukia na asiweze kutangamana naye kwa wema, basi inafaa kwake kumrudishia yale aliyompa. Hakuna ubaya kwa mke kumrudishia na wala hakuna ubaya kwa mume kumkubalia.”[2]

Jambo hili linaitwa Khul´.

[1] 02:229

[2] (01/483).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tanbiyhaat, uk. 109-110
  • Imechapishwa: 25/11/2019