60. Kila kitu kumewepesishwa


Abu Muhammad ´Abdullaah bin Abiy Zayd al-Qayrawaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

Kutokana na ujuzi na makadirio Yake yaliyokwishatangulia kila mmoja amewepesishiwa juu ya kula maangamivu au furaha.

MAELEZO

Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) walisema:

“Ee Mtume wa Allaah! Yale tunayofanya yamekwishapangwa au hayajapangwa?” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Yamekwishapangwa.” Maswahabah wakasema: “Si tutegemee basi tuliyoandikiwa na tuache kutenda?” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Fanyeni matendo! Kwani hakika kila mmoja ni mwenye kufanyiwa wepesi juu ya kile alichoumbiwa.” Kisha akasoma:

فَأَمَّا مَنْ أَعْطَىٰ وَاتَّقَىٰ وَصَدَّقَ بِالْحُسْنَىٰ فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْيُسْرَىٰ وَأَمَّا مَن بَخِلَ وَاسْتَغْنَىٰ وَكَذَّبَ بِالْحُسْنَىٰ فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْعُسْرَىٰ

“Basi yule anayetoa na akamcha Allaah na akasadikisha lililo jema zaidi, basi tutamuwepesishia kwa yaliyo mepesi. Ama yule afanyaye ubakhili na akajiona amejitosheleza na akakadhibisha lililo jema zaidi, basi tutamuwepesishia kwa yaliyo magumu.”[1]

Akabainisha (Subhaanah) kwamba uongofu na upotofu yanatokamana na mja, jambo ambalo ni uadilifu na fadhilah za Allaah.

[1] 92:5-10 al-Bukhaariy (4949) na Muslim (2647).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 48
  • Imechapishwa: 05/08/2021