60. Fadhila za Sujuud


Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna yeyote kutoka katika Ummah wangu isipokuwa nitamjua siku ya Qiyaamah.” Wakasema: “Ee Mtume wa Allaah! Utawezaje kufanya hivo katika umati wa watu?” Akasema: “Unaonaje iwapo utaingia kwenye boma ambapo kuna farasi weusi tii na farasi mwengine ana alama nyeupe kwenye paji lake na uso na miguuni mwake; hutomjua?” Mtu yule akasema: “Ndio.” Ndipo akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Hakika Ummah wangu watakuwa na weupe wa Sujuud na wudhuu[1]´.”[2]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Pindi Allaah atapotaka kuwahurumia waliyomo Motoni basi Anawaamrisha Malaika wawatoe wale waliokuwa wakimuabudu Allaah. Wawatoe na watawajua kutokana na athari ya Sujuud. Allaah ameuharamishia Moto kuunguza athari ya Sujuud. Hivyo watoke Motoni. Moto unaunguza kila kitu kwa mwanaadamu isipokuwa tu athari ya Sujuud.”[3]

[1] Bi maana viungo vya mwili vinavyooshwa wakati wa wudhuu´: mikono, uso na miguu. Kadhalika farasi ana weupe usoni mwake pamoja na sehemu ya unyayo wake wa mbele na wa nyuma. Tazama “an-Nihaayah”.

[2] Ahmad kwa mlolongo wa wapokezi mzuri. Kadhalika at-Tirmidhiy amepokea baadhi yake na akaisahihisha. Imetajwa katika “as-Swahiyhah”.

[3] al-Bukhaariy na Muslim. Hadiyth inathibitisha ya kwamba wale waswaliji watenda madhambi hawatobaki Motoni. Bali hata wale wapwekeshaji wenye kuiacha kwa sababu ya uvivu. Hatobakizwa humo. Hii ni sahihi. Tazama “as-Swahiyhah” (2054).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 129-130
  • Imechapishwa: 04/08/2017