60. al-Qummiy upotoshaji wake wa tatu wa Aal ´Imraan

al-Qummiy amesema pindi alipokuwa akifasiri Aayah:

أَفَغَيْرَ دِينِ اللَّـهِ يَبْغُونَ

“Je, wanataka dini isiyokuwa ya Allaah?”[1]

“Je, wanataka kitu kingine kisichokuwa hichi nilichowaamrisha wamkubali Muhammad na wausiwa wake?

وَلَهُ أَسْلَمَ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ طَوْعًا وَكَرْهًا

“Amejisalimisha Kwake kila aliye katika mbingu na katika ardhi akipenda asipende.”

“Kutokamana na woga wa upanga.”[2]

Tazama namna ambavyo mwongo huu anaupoteza Uislamu na maana kubwa ya Qur-aan na malengo yake makubwa. Dini ya Allaah imekusanya yale yote aliyokuja nayo Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika ´Aqiydah, ´ibaadah, matendo, hukumu, Jihaad, uadilifu, wema, makatazo ya shirki, maovu na mambo ya shari. Ujumbe wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) unakusanya kumuamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Qadar na Qiyaamah na nguzo za Uislamu shahaadah, swalah, swawm, zakaah na hajj. Baatwiniy huyu anapoteza misingi yote hii mikubwa na matendo matukufu na kuifanya Aayah (ambayo imekusanya mambo yote haya yaliyotajwa) ni yenye kukomeka na kushuhudia wasia wa ´Aliy ambao isitoshe umezuliwa na myahudi Ibn Sabaa´. Hakumtaja Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) isipokuwa tu ni kwa ajili ya kutaka kuficha ukafiri huu.

Kuhusiana na tafsiri yake:

وَلَهُ أَسْلَمَ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ طَوْعًا وَكَرْهًا

“Amejisalimisha Kwake kila aliye katika mbingu na katika ardhi akipenda asipende.”

ni ya kimakosa. Kujisalimisha kwa kupenda na kwa kutokupenda ni kule kunyenyekea kwa maamrisho ya kilimwengu na ya kimakadirio kwa Allaah. Kila kilichomo mbinguni na ardhini ni chenye kunyenyekea matakwa na makadirio ya Allaah. Hakuna anaeyakwepa. Kana kwamba anachomaanisha ni kuwa kila kilichomo mbinguni na ardhini ni chenye kunyenyekea kwa woga sawa kwa kupenda au kwa kutokupenda upanga wa ´Aliy. Wala haishangazi kabisa Baatwiniy huyu akawa anamaanisha hivo.

[1] 03:83

[2] Tafsiyr al-Qummiy (1/107).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 98
  • Imechapishwa: 03/04/2017