60. Afanye nini mwanamke akiona mume wake hamtamani na yeye anapenda kubaki pamoja naye?

Allaah (Ta´ala) amesema:

وَإِنِ امْرَأَةٌ خَافَتْ مِن بَعْلِهَا نُشُوزًا أَوْ إِعْرَاضًا فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا أَن يُصْلِحَا بَيْنَهُمَا صُلْحًا ۚ وَالصُّلْحُ خَيْرٌ

“Na ikiwa mke atachelea kutoka kwa mumewe uonevu wa ndoa au kutengwa, basi hakuna neno juu yake wakisikilizana kati yao kwa suluhu – na suluhu ni bora.”[1]

Haafidhw Ibn Kathiyr amesema:

“Mwanamke akichelea mume wake kumkimbia au kumpa mgongo, basi inafaa kwake kudondosha kutoka kwa mume huyo haki zake au baadhi ya haki zake kama vile matumizi, mavazi, makazi au haki nyenginezo zilizo juu ya mume. Inafaa pia kwa mume kukubali hayo kutoka kwake mke. Hakuna ubaya kwa mke kujitolea mambo hayo na wala hakuna ubaya kwa mume kumkubalia. Kwa ajili hiyo amesema:

 فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا أَن يُصْلِحَا بَيْنَهُمَا صُلْحًا ۚ وَالصُّلْحُ خَيْرٌ

“Basi hakuna neno juu yake wakisikilizana kati yao kwa suluhu – na suluhu ni bora.”[2]

Bi maana ni bora kuliko kuachana. Kisha akataja kisa cha Sawdah bint Zam´ah (Radhiya Allaahu ´anhaa) na kwamba alipokuwa mtumzima na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaazimia kumwacha, akalitatua kwa yeye kubaki naye na akajitolea siku yake kumpa ´Aaishah ambapo akamkubalia hilo kutoka kwake na akambakiza juu ya hayo.”[3]

[1] 04:128

[2] 04:128

[3] (02/402).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tanbiyhaat, uk. 109
  • Imechapishwa: 25/11/2019