6. Vidhibiti vya majina Saudi Arabia

Linaloshangaza zaidi kuliko hivo ni kuwa huwezi kuona makafiri wenye majina ambayo ni maalum kwa waislamu. Makafiri wanajitukuza kwa hili – na ni jambo lenye kulaumika. Hata hivyo kujitukuza kwa muislamu ni jambo lenye kusifiwa na linalotakikana. Vipi basi tupuuzie hilo? Vipi tunaweza kuwafuata maadui zetu? Vipi tunaweza kufuata njia yao na kuacha njia yetu? Hakuna uwezo wala nguvu isipokuwa kupitia kwa Allaah, Mwenye nguvu, Mwenye hekima.

Pamoja na majanga na makosa haya kuna vigezo vyenye kusitisha mwendelezo na kulinda mpaka huu. Kwanza ni Allaah (Ta´ala) ndiye anastahiki kushukuriwa kwa hilo kisha watu wenye kulinda dini na Shari´ah Yake. Katika roho ya kisiwa cha Kiarabu kuna vidhibiti vya jina:

1- Ni lazima liendane sambamba na Shari´ah.

2- Ni marufuku kabisa kutoa jina lisiloafikiana na Shari´ah.

3- Majina ya mara mbili yamepigiwa marufuku kutokana na ukhofiaji wa uchanganyikiwaji.

4- Ni lazima ukoo uambatanishwe na “bin” (mtoto wa) kati ya majina.

  • Mhusika: ´Allaamah Bakr bin ´Abdillaah Abu Zayd
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasmiyat-ul-Mawluwd, uk. 06-07
  • Imechapishwa: 18/03/2017