6. Uso wa mwanamke ni wenye fitina zaidi kuliko sauti ya mnyororo wake

Ya tano: Allaah (Ta´ala) amesema:

وَلَا يَضْرِبْنَ بِأَرْجُلِهِنَّ لِيُعْلَمَ مَا يُخْفِينَ مِن زِينَتِهِنَّ

“Na wala wasipige miguu yao [wanapotembea] yajulikane yale wanayoyaficha katika mapambo yao.”

Hii ina maana ya kwamba haitakiwi kwa mwanamke kupiga miguu wanaume wakaja kujua kuwa amevaa minyororo na mapambo mengine. Ikiwa mwanamke amekatazwa kupiga miguu ili asije akawafitinisha wanaume kwa sauti ya minyororo na mengineyo, basi ni jambo lililo la khatari zaidi kwa uso uliofunuliwa. Ni kipi kilicho na fitina na kuvutia zaidi mwanaume kusikia sauti ya mnyororo wa mwanamke asiyejua kama ni kijana au mzee, mbaya au mzuri, au kuona uso wake uliofunuliwa, mzuri, mwembamba, wenye kung´aa na mzuri? Wanaume wote wenye kuvutikiwa na wanawake wanajua ni kipi chenye fitina zaidi na kilicho muhimu zaidi kufunikwa na kufichikwa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hijaab, uk. 9-10
  • Imechapishwa: 26/03/2017