Kuwepo kwa baadhi ya wanazuoni wenye kudai ya kwamba kuna Bid´ah nzuri ni jambo linaloingia katika moja kati ya mambo mawili:

1 – Kitendo kiwe si Bid´ah kabisa tofauti na wanavyodhania.

2 – Kitendo kiwe ni Bid´ah mbaya pasi na wao kujua ubaya wake.

Kila mwenye kudai ya kwamba kuna Bid´ah ilio nzuri anajibiwa namna hii. Kutokana na hilo Ahl-ul-Bid´ah hawana bahati yoyote ile ya kufanya na kudai Bid´ah nzuri na sisi tumeshikamana na upanga ulio mkali wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ninakutahadharisheni na mambo yaliyozuliwa, kwani hakika kila kitakachozushwa ni Bid´ah na kila Bid´ah ni upotevu na kila upotevu ni Motoni.”

Upanga huu mkali umenolewa na ulinganizi na ujumbe wa kiutume na si kwa maneno ya kipuuzi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameunoa kwa njia yenye kugonga kwa njia ya kwamba hakuna yeyote mwenye kudai Bid´ah nzuri anaweza kukabiliana na mtu ambaye ameshika upanga huu mkali ulionolewa ipasavyo. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ninakutahadharisheni na mambo yaliyozuliwa, kwani hakika kila kitakachozushwa ni Bid´ah na kila Bid´ah ni upotevu na kila upotevu ni Motoni.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ibdaa´ fiy Kamaal-ish-Shar´ wa Khatwar-il-Ibtidaa´, uk. 8-9
  • Imechapishwa: 23/10/2016