Shaykh (Rahimahu Allaah) aliulizwa swali:

“Unasemaje juu ya yule mwenye kusema kwamba Shaykh Rabiy´ ana papara na haraka?”

Akajibu (Rahimahu Allaha):

“Shaykh Rabiy´ ana uzowefu wa kutambua hali halisi kwa sababu aliishi pamoja na al-Ikhwaan al-Muslimuun kwa muda mrefu[1]. Yeye ni mbora – na himdi zote ni Zake Allaah – wa kuyatatua mambo haya na kuraddi Bid´ah za watu wa Bid´ah. Ninamuomba Allaah Amuhifadhi.”[2]

Amesema (Rahimahu Allaah) pia:

“Miongoni mwa watu leo walio na uoni wa mbali na ujuzi kuhusu makundi na matawi ya makundi, ni ndugu Shaykh Rabiy´ bin Haadiy (Hafidhwahu Allaah). Wakati Shaykh Rabiy´ anaposema kuwa mtu fulani ni “Hizbiy”, itakuja kufichuka siku moja kweli kwamba ni Hizbiy. Mtakuja kukumbuka hilo. Inahusiana tu na kwamba mtu huyo mwanzoni jambo lake litakuwa halijulikani na kwa ajili hiyo ndio maana hataki hali yake iweze kujulikana. Hata hivyo hili hubadilika wakati anapopata nguvu na akawa na wafuasi na wakati huohuo anaonelea kuwa hadhuriki kwa kuzungumzwa vibaya. Kwa ajili hiyo ndio maana nashauri mtu kusoma vitabu vyake (Hafidhwahu Allaah) na kustafidi navyo.”[3]

Amesema pia (Rahimahu Allaah):

“Himdi zote ni Zake Allaah Ahl-us-Sunnah wanaikwamua jamii kwa njia ya kihakika.

“Hakutoacha kuwepo daima kundi katika Ummah wangu likiwa ni lenye kushinda juu ya haki. Hawatodhurika na wale wenye kwenda kinyume nao wala wale wenye kuwakosesha nusura mpaka ifike amri ya Allaah na wao bado wako katika hali hiyo.”

Shaykh Rabiy´ yuko katika ardhi ya Misikiti miwili Mitakatifu na Najd. Ndio, himdi zote ni Zake Allaah. Anawakwamua kwa njia ya kihakika na kubainisha yale waliyomo.”[4]

Shaykh (Rahimahu Allaah) amesema vilevile katika jibu la swali:

“Ninawanasihi ndugu kustafidi katika vitabu vya ndugu yetu Shaykh Rabiy´ bin Haadiy (Hafidhwahu Allaah). Ana uoni wa mbali na ujuzi kuhusu Hizbiyyuun. Anafungua Hizbiyyah kwa patasi. Baadhi ya watu wamesema kuwa baadhi ya taaliki ya kitabu “al-Kashshaaf” zinafungua I´tizaal zake kwa patasi. Kadhalika Hizbiyyah inafunguka kwa patasi. Ninawanasihi kustafidi kutoka kwenye vitabu vyake na kadhalika kanda zake.”

Amesema vilevile:

“Ninanasihi kusoma kitabu cha ndugu yetu Rabiy´ bin Haadiy “Jamaa´ah Waahidah laa Jamaa´aat wa Swiraatw Waahidah laa ´Asharaat”. Kitabu hicho kinatosheleza.”

Halafu akasema:

“Tunashauri wawatumie barua wanachuoni. Ikiwa mtu yuko na uwezo, anatakiwa kusafiri kwenda kwao, kwa mfano Shaykh al-Albaaniy, Shaykh Ibn Baaz, Shaykh ´Abdul-Muhsin al-´Abbaad, Shaykh Rabiy´ bin Haadiy na Shaykh Ibn ´Uthaymiyn. Ikiwa watu wako na uwezo wa kusafiri kuwaendea, basi wafanye hivo. Ikiwa hawawezi kufanya hivo, wawe na mawasiliano nao kwa njia ya simu na kuwatumia barua.”[5]

Amesema pia wakati alipoulizwa juu ya ni wanachuoni gani mtu anatakiwa kuwarejelea:

“Shaykh Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy. Ni alama miongoni mwa alama za Allaah (Aayatullaah) katika elimu na kuwatambua Hizbiyyuun. Lakini hata hivyo sio kama alama Dajjaal wa Iraan.”[6]

Aliulizwa swali pia:

“Ni wanachuoni gani wa kisaudi unatushauri kuchukua elimu kwao? Unaweza kututajia baadhi ya majina?”

Akajibu:

“Wale ninaowajua ambao ninanasihi kuchukua elimu kwao. Miongoni mwao ni Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz (Hafidhwahu Allaah), Shaykh Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn (Hafidhwahu Allaah), Shaykh Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy (Hafidhwahu Allaah) na Shaykh ´Abdul-Muhsin al-´Abbaad (Hafidhwahu Allaah). Kadhalika Shaykh Swaalih al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah) anasemwa vizuri, hata kama simjui. Mtu anaweza kila siku kumuomba ushauri Shaykh Ibn Baaz kwa kuwa yeye ni mjuzi zaidi. Ni kitambo nilikuwa katika nchi hiyo.”[7]

 Amesema wakati alipokuwa akizungumzia juu ya ´Abdur-Rahmaan ´Abdul-Khaaliq:

“Mimi naonelea kuwa hastahiki kuraddiwa. Lakini himdi zote ni Zake Allaah kwamba Shaykh Rabiy´ (Hafidhwahu Allaah) amefanya ambayo Allaah Amemuwajibishia juu yake kufanya. Anatakiwa kushukuriwa kwa hilo.”[8]

Amesema pia:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakutoacha kuwepo daima kundi katika Ummah wangu likiwa ni lenye kushinda juu ya haki. Hawatodhurika na wale wenye kwenda kinyume nao wala wale wenye kuwakosesha nusura mpaka ifike amri ya Allaah na wao bado wako katika hali hiyo.”

Miongoni mwa wanachuoni hawa ni Shaykh Ibn Baaz (Hafidhwahu Allaah), Shaykh al-Albaaniy (Hafidhwahu Allaah), Shaykh Swaalih al-Fawzaan, Shaykh Rabiy´ bin Haadiy na Shaykh ´Abdul-Muhsin al-´Abbaad (Hafidhwahu Allaah).”[9]

Katika kitabu hichohicho kwa anwani “Ni nani alie nyuma ya ulipuaji katika ardhi ya Misikiti miwili Mitakatifu?” Shaykh Muqbil aliwanasihi watu wa Kuwait yafuatayo:

“Kadhalika ninawanasihi kumwalika ndugu yetu Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy Kuwait, ili aweze kubainisha upotevu wa ´Abdur-Rahmaan ´Abdul-Khaaliq, Suruuriyyah na Qutbiyyah.”

Katika dibaji ya kitabu cha Muhammad al-Imaam “Tanwiyr-udh-Dhwulumaat”, uk. 6, amesema yafuatayo:

“Hizbiyyuun wengi walikuwa na nguvu, mamlaka na bali majina makubwa. Baada ya Ahl-us-Sunnah kubainisha hali zao, wakafa wao na fikira zao zikafa. Miongoni mwa wanachuoni watukufu wa leo wanaokabiliana na watu wa batili ni Shaykh Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy (Rahimahu Allaah), Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz (Rahimahu Allaah), Shaykh Rabiy´ bin Haadiy na wengineo.”

Ameusia (Rahimahu Allaah) katika jibu la swali la vijana wa Qatar wawaalike wanachuoni. Miongoni mwao ilikuwa ni Shaykh Rabiy´ na akawanasihi wasafiri kwenda kwake kutafuta elimu.

Shaykh Muqbil (Rahimahu Allaah) alikuwa akimsifu na akimuadhimisha maadhimisho makubwa. Kipindi ambacho alikuwa amelazwa mgonjwa Hospitali Makkah na Juddah nilihudhuria mikutano yao mingi. Kulikuwepo mapenzi ya hali ya juu na ya kidugu, heshima na maadhimisho kati yao. Kila wakati Shaykh Muqbil akipata fursa alikuwa akimtembelea Shaykh nyumbani kwake.

Ndugu na Shaykh ´Abdul-´Aziyz al-Bura´iy amesema katika kalima yake kwa anwani “adh-Dhabb ´an as-Sunnah wa ´Ulaaihaa”:

“Mashaykh wane al-Albaaniy, Ibn Baaz, Muqbil na Ibn ´Uthaymiyn wamekufa hali ya kuwa wote walikuwa radhi na wenye kuridhika na hali ya Da´wah na njia ambayo Shaykh Rabiy´ anafanya Da´wah yake katika Uislamu. Siku moja Shaykh Rabiy´ aliingia kwenye nyumba ambayo Shaykh Muqbil alikuwa akiishiemo Makkah na tulikuwa pamoja naye. Shaykh Rabiy´ akawasalimia waliokuwepo pale mpaka alipofika kwa Shaykh Muqbil ambaye alikuwa amekaa na akasema kumwambia:

“Wewe ni mtu unayestahiki kusimamiwa, lakini naumwa.”

Katika maadhimisho ya Shaykh Rabiy´ kwa Shaykh Muqbil ni yale niliyoyaona wakati nilipokuwa na Shaykh Rabiy´ kwenda kumtembelea Shaykh Muqbil Hospitali Juddah baada ya kurudi kwake kutoka katika matibabu Ujerumani. Wakati tulipofika chumbani kwake Shaykh alikuwa amelala kwenye koma katika kitanda chake. Shaykh Rabiy´ akasogea mbele, akambusu paji lake la uso na akalia sana. Allaah Amrehemu kwa Rahmah kunjunfu na Atujumuishe sisi na wanachuoni wetu katika Pepo yake yenye neema.

[1] Huenda Shaykh anachokusudia hapa ni kwamba Shaykh aliishi karibu nao na kutumia muda fulani katika kubainisha upotevu wao. Kutokana na sababu hii ndio maana akawa na uzowefu wa upotevu wao na hali yao ya kweli. Shaykh Rabiy´ hajawahi hata siku moja kuwa katika al-Ikhwaan alMuslimuun. Hata hivyo alienda nao ili kuwanyoosha na kuwa pamoja nao kwa masharti ambayo kamwe hawakuyatimiza. Yote hayo yanabainika pale ambapo Shaykh Rabiy´ alijieleza katika Radd yake kwa ´Abdur-Rahmaan ´Abdul-Khaaliq: ”Jambo la kwanza nilitumia muda nikiwa pamoja na al-Ikhwaan al-Muslimuun, lakini kwa nini? Ndio, kwa ajili ya kuwanyoosha na kuwalea juu ya mfumo wa Salaf na sio kwa ajili ya maslahi ya kidunia. Nilienda nao kwa masharti mawili kutimizwa. Sharti ya kwanza mfumo ambao wanatakiwa kupita juu yake na kulea harakati zao ulimwenguni uwe ni mfumo wa Salaf. Sharti ya pili ilikuwa ni kusibaki mtu wa Bid´ah yoyote katika safu yao, na khaswa ikiwa inahusiana na Bid´ah kubwa na ya khatari. Wakakubaliana na masharti yangu. Walionifanya kwenda na kunikubalia masharti yangu, ilikuwa ni watu ambao nilikuwa naamini kuwa ni Salafiyyuun na wangelinisaidia kutimiza masharti niliyoyaweka. Nikaanza kusubiri masharti haya yatimizwe na kuwataka wayahakikishe hali ya kuwa ni mwenye subira muda mrefu. Nikavumilia wakati mambo kila siku bado yako pale pale. Ndipo kulipodhihiri mirengo ya ki-Suufiy yenye nguvu ambayo ilijitokeza kupitia baadhi ya vigogo wa Suufiyyah na vitabu vyao, jambo likapelekea kuwa ni sababu ya wao kugeuka kwenda katika vitabu hivi vya ki-Suufiy na kuupa mfumo wa Salaf mgongo. Hivyo wakaonesha wazi vita vyao dhidi ya Salafiyyah na Salafiyyuun. Wakati nilipofika katika kilele cha mwisho na kuona kunadhihiri kuoneana huruma pamoja na Rawaafidhw, nikaona kuwa haijuzu tena kwangu kubaki na wao. Kwa hivyo, nilienda nao kwa ajili ya Allaah na nikatoka kwa ajili ya Allaah. Ninamuomba Allaah msamaha kwa madhambi na mapungufu yangu kwa muda niliutumia pamoja nao.” (Tazama ”an-Naswr al-´Aziyz”, uk. 187- 188)

[2] Kanda ”al-As-ilah al-Hadhwramiyyah”.

[3] Kanda ”al-As-ilah as-Sunniyyah li ´Allaamah ad-Diyaar al-Yamaniyyah – As-ilah Shabaab at-Twaaif”.

[4] Kanda ”Thanaa´-ul-´Ulamaa´ ´alaa ash-Shaykh Rabiy´”

[5] Swali la 123.

[6] Swali la 135.

[7] Swali la 140.

[8] Swali la 144

[9] Swali la 162.

  • Mhusika: Shaykh Khaalid bin Dhwahwiy adh-Dhwafayriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.rabee.net/ar/sharticles.php?cat=12&id=57
  • Imechapishwa: 02/12/2019