Swali: Allaah (Ta´ala) amesema:

لَّا يَمَسُّهُ إِلَّا الْمُطَهَّرُونَ

“Haigusi isipokuwa waliotakaswa kabisa.”[1]

Je, hili ni jambo linalowahusu waislamu peke yao pasi na makafiri hata kama makafiri hao watakuwa wasafi?

Jibu: Imesemekana kwamba:

لَّا يَمَسُّهُ إِلَّا الْمُطَهَّرُونَ

“Haigusi isipokuwa waliotakaswa kabisa.”[2]

wanaokusudiwa ni Malaika. Kuna maoni vilevile yanayosema kwamba inawahusu vilevile wanaadamu. Wako ambao wanaona kuwa Qur-aan haiguswi isipokuwa na ambaye ametawadha. Dalili juu ya hilo ni ile barua ambayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwandikia ´Amr bin Hamz:

“Asiiguse Qur-aan isipokuwa aliye msafi.”

Japokuwa tafsiri ya Aayah hapo juu inahusu Ubao uliohifadhiwa na wagusaji hapo ni Malaika lakini kadhalika Qur-aan haitakiwi kuguswa isipokuwa na ambaye ametawadha.

Kuhusu kafiri hatakiwi kuigusa Qur-aan wala hatakiwi kuachwa akaigusa.

[1] 56:79

[2] 56:79

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (05) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191110#219240
  • Imechapishwa: 21/09/2019