59. Ni ipi Sunnah kwa mwenye kufuata jeneza?


Swali 59: Ni ipi Sunnah kwa mwenye kufuata jeneza[1]?

Jibu: Sunnah kwa anayefuata jeneza ni yeye asiketi chini mpaka jeneza litue chini ardhini. Ama kundoka kilichowekwa katika Shari´ah ni mtu asiondoke mpaka maiti awekwe ndani ya kaburi na wamalize kuzika. Yote haya kwa njia ya mapendekezo. Lakini bora kwa ambaye amefuata mazishi asiondoke isipokuwa baada ya kumaliza kuzika ili akamilishe ujira mara mbili; ujira wa swalah na ujira usindikizaji. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote atakayefuata jeneza la muislamu hali ya kuwa na imani na kutarajia malipo kutoka kwa Allaah na akawa pamoja nalo mpaka akamswalia na wakamaliza kumzika, basi anarejea akiwa na Qiraatw mbili. Kila Qiraatw moja ni mfano na mlima wa Uhud.”[2]

Ameipokea al-Bukhaariy katika “as-Swahiyh” yake.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/177-178).

[2] al-Bukhaariy (47).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 44-45
  • Imechapishwa: 26/12/2021