59. Makatazo ya muislamu kuishi katika miji ya makafiri

5- Miongoni mwa hukumu zinazopelekea katika kuwakufurisha makafiri ni kujitenga nao mbali na ni wajibu kwa muislamu kuhama kutoka katika nchi zao. Ni wajibu kwa muislamu ambaye hawezi kudhihirisha dini yake kuhama na kwenda katika mji wa Kiislamu kama alivyohama Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah wake kwa ajili ya kulinda dini yao. Muislamu hatakiwi kubaki katika mji wa makafiri ikiwa hawezi kuidhihirisha dini yake. Amesema (Subhaanahu wa Ta´ala):

إِنَّ الَّذِينَ تَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ ظَالِمِي أَنفُسِهِمْ قَالُوا فِيمَ كُنتُمْ ۖ قَالُوا كُنَّا مُسْتَضْعَفِينَ فِي الْأَرْضِ ۚ قَالُوا أَلَمْ تَكُنْ أَرْضُ اللَّـهِ وَاسِعَةً فَتُهَاجِرُوا فِيهَا ۚ فَأُولَـٰئِكَ مَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ ۖوَسَاءَتْ مَصِيرًا لَّا الْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاءِ وَالْوِلْدَانِ لَا يَسْتَطِيعُونَ حِيلَةً وَلَا يَهْتَدُونَ سَبِيلًا  فَأُولَـٰئِكَ عَسَى اللَّـهُ أَن يَعْفُوَ عَنْهُمْ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَفُوًّا غَفُورًا

”Hakika wale ambao Malaika wamewafisha hali wamejidhulumu nafsi zao [Malaika] watawauliza: “Mlikuwa katika hali gani?” Watasema: “Tulikuwa tukikandamizwa katika ardhi.”  Watasema: “Je, kwani ardhi ya Allaah haikuwa pana mkahajiri?” Basi hao makazi yao yatakuwa ni [Moto wa] Jahannam – na ubaya ulioje mahali pa kurejea! Isipokuwa wale waliokandamizwa kati ya wanaume na wanawake na watoto ambao hawakuweza kupata namna yoyote wala hawawezi kuongoza njia. Basi hao huenda Allaah akawasamehe. Allaah ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kughufiria.” (an-Nisaa´ 04: 97-99)

“Mimi nimejitenga mbali na yule mwenye kuishi baina ya migongo ya washirikina.”[1]Yule asiyeweza kuhama ni mwenye kupewa udhuru. Lakini kwa yule mwenye kuweza, basi huyu ni wajibu kwake kuhama. Haijuzu kwake kuishi baina ya migongo ya washirikina. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

Ni wajibu kwa muislamu, ambaye hawezi kudhihirisha dini yake, ahame.

Hijrah imeambatanishwa pamoja na kupigana Jihaad katika njia ya Allaah (´Azza wa Jall). Imetajwa sambamba pamoja na Jihaad. Amesema (Ta´ala):

إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَالَّذِينَ هَاجَرُوا وَجَاهَدُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ

”Hakika wale walioamini na wale waliohajiri na wakapigana Jihaad katika njia ya Allaah.”(al-Baqarah 02:218)

Hijrah jambo lake ni kuu katika Uislamu. Hijrah ni kule kuhama kutoka katika nchi ya kikafiri kwenda katika nchi ya waislamu kwa ajili ya kuilinda dini.Kwa hivyo ni wajibu kwa yule ambaye hawezi kudhihirisha dini yake kuhama.

[1] Ameipokea Abu Daawuud (2645), at-Tirmidhiy (1604) na an-Nasaa´iy (4780).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 87-89
  • Imechapishwa: 16/10/2018