58. Ni ipi Sunnah katika kumsindikiza maiti?


Swali 58: Ni ipi Sunnah katika kumsindikiza maiti[1]?

Jibu: Sunnah ni kwamba yule msindikizaji amfuate kutoka nyumbani kwenda sehemu ya kuswalia na kutoka sehemu ya kuswalia kwenda makaburini. Abaki pamoja naye mpaka wamalize kumzika. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yeyote atakayefuata jeneza la muislamu hali ya kuwa na imani na kutarajia malipo kutoka kwa Allaah na akawa pamoja nalo mpaka akamswalia na wakamaliza kumzika, basi anarejea akiwa na Qiraatw mbili. Kila Qiraatw moja ni mfano na mlima wa Uhud.”[2]

Ameipokea al-Bukhaariy katika “as-Swahiyh” yake.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/177).

[2] al-Bukhaariy (47).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 43-44
  • Imechapishwa: 26/12/2021