Ee mwanamke wa Kiislamu! Ni lazima kwako kumtii mume wako kwa wema. Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ataposwali mwanamke vipindi vyake vitano, akahifadhi tupu yake na akamtii mume wake, basi ataingia kupitia mlango wowote wa Peponi anaotaka.”

Ameipokea Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh” yake.

Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Si halali kwa mwanamke kufunga na mume wake yuko isipokuwa kwa idhini yake.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mume atapomwita mke wake kitandani na asije akalala na huku amemkasirikia, basi hulaaniwa na Malaika mpaka kupambazuke.”

Ameipokea al-Bukhaariy, Muslim na wengineo.

Katika upokezi wa al-Bukhaariy na Muslim Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ninaapa kwa ambaye nafsi yangu iko mikononi Mwake. Hakuna mwanamume ambaye anamwita mke wake kitandani ambapo akamkatalia isipokuwa Ambaye yuko juu ya mbingu humkasirikia.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tanbiyhaat, uk. 106-107
  • Imechapishwa: 20/11/2019