58. Makatazo ya kusoma Qur-aan katika Sujuud

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kusoma Qur-aan katika Rukuu´ na Sujuud. Ameamrisha kujitahidi na kukithirisha kuomba du´aa katika nguzo hii, kama ilivyotajwa katika Rukuu´. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mja anakuwa karibu zaidi na Mola wake anapokuwa amesujudu. Hivyo basi kithirisheni du´aa.”[1]

[1] Muslim, Abu ´Awaanah na al-Bayhaqiy. Imetajwa katika ”al-Irwaa’” (456).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 128
  • Imechapishwa: 04/08/2017