58. Makatazo ya kumuozesha dada wa Kiislamu kwa mwanaume wa kikafiri

4- Haijuzu mwanamke wa Kiislamu kumuozesha kwa kafiri kwa kuchelea dini ya mwanamke huyo ili asije kuwa chini ya mamlaka yake. Amesema (Subhaanahu wa Ta´ala):

وَلَا تَنكِحُوا الْمُشْرِكَاتِ حَتَّىٰ يُؤْمِنَّ ۚ وَلَأَمَةٌ مُّؤْمِنَةٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكَةٍ وَلَوْ أَعْجَبَتْكُمْ

”Wala msiwaoe wanawake washirikina mpaka waamini. Mjakazi muumini ni bora kuliko mshirikina japo akikupendezeni.” (al-Baqarah 02:221)

فَإِنْ عَلِمْتُمُوهُنَّ مُؤْمِنَاتٍ فَلَا تَرْجِعُوهُنَّ إِلَى الْكُفَّارِ ۖ لَا هُنَّ حِلٌّ لَّهُمْ وَلَا هُمْ يَحِلُّونَ لَهُنَّ

”Mkiwatambua kuwa ni waumini wa kike, basi msiwarejeshe [huko Makkah] kwa makafiri; wao [wanawake] si halali kwao [makafiri] na wala wao [waume] si halali kwao [hao wanawake].” (al-Mumtahinah 60:10)

Haijuzu dada wa Kiislamu kuozeshwa kwa kafiri kwa hali yoyote kabisa. Ni mamoja kafiri huyo ni myahudi, mnaswara wala mshirikina. Inahusiana na makafiri wote.

Ama kuhusu muislamu wa kiume kumuoa mwanamke wa kikafiri, ikiwa mwanamke huyo ni mwabudu masanamu na mshirikina, basi haijuzu kwa muislamu kumuoa. Amesema (Ta´ala):

وَلَا تَنكِحُوا الْمُشْرِكَاتِ حَتَّىٰ يُؤْمِنَّ ۚ وَلَأَمَةٌ مُّؤْمِنَةٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكَةٍ وَلَوْ أَعْجَبَتْكُمْ ۗ وَلَا تُنكِحُوا الْمُشْرِكِينَ حَتَّىٰ يُؤْمِنُوا ۚ وَلَعَبْدٌ مُّؤْمِنٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكٍ وَلَوْ أَعْجَبَكُمْ ۗأُولَـٰئِكَ يَدْعُونَ إِلَى النَّارِ ۖ وَاللَّـهُ يَدْعُو إِلَى الْجَنَّةِ وَالْمَغْفِرَةِ بِإِذْنِهِ

”Wala msiwaoe wanawake washirikina mpaka waamini. Mjakazi muumini ni bora kuliko mshirikina japo akikupendezeni. Wala msiwaoze wanaume washirikina mpaka waamini. Mtumwa muumini ni bora kuliko mshirikina japo akikupendezeni – hao wanaita katika Moto na Allaah anaita katika Pepo na msamaha kwa idhini Yake.”(al-Baqarah 02:221)

Ama mwanamke huyo ni ima myahudi au mnaswara, inajuzu kwa muislamu kumuoa kwa sharti awe ni mtwaharifu na mwenye kujiheshimu katika heshima yake. Amesema (Ta´ala):

وَطَعَامُ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ حِلٌّ لَّكُمْ وَطَعَامُكُمْ حِلٌّ لَّهُمْ ۖ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الْمُؤْمِنَاتِ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلِكُمْ

“… na chakula cha wale waliopewa Kitabu ni halali kwenu na chakula chenu ni halali kwao na wanawake watakasifu miongoni mwa waumini wanawake na wanawake watakasifu miongoni mwa wale waliopewa Kitabu kabla yenu… “ (al-Maaidah 05:05)

Makusudio ya neno ´al-Muhswanah` ni yule mtwaharifu kutokamana na uzinzi. Kuhusu wale wanawake wa kinaswara ambao wanasifika kwa uzinzi au uasherati, huyu haijuzu kwa muislamu kumuoa, isipokuwa anatakiwa kumuoa mwanamke wa kiyahudi au wa kinaswara ambao ni wasafi katika heshima zao na wametakasika na uzinzi. Kwa sababu mwanamke huyu anakuwa chini ya usimamizi wa mwanaume. Atapokuwa chini ya usimamizi wake huenda mwanamke huyo akasalimu. Hapa mamlaka ya muislamu ndio yanakuwa juu ya mwanamke kafiri. Lakini kinyume haifai. Mamlaka ya kafiri hayawi juu ya mwanamke wa Kiislamu. Amesema (Ta´ala):

وَلَن يَجْعَلَ اللَّـهُ لِلْكَافِرِينَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ سَبِيلًا

“Allaah hatojaalia njia kwa makafiri juu ya waumini.”(an-Nisaa´ 04:141)

Haya ndio maelezo kuhusu kuoana kati ya waislamu na makafiri. Mwanamke akiwa ni kafiri, mwabudu masanamu, mkanamungu au aliyeritadi, basi haijuzu kwa muislamu kumuoa kabisa. Ama akiwa ni katika Ahl-ul-Kitaab itafaa kumuoa kwa sharti awe mtwaharifu na msafi kutokamana na uzinzi. Hilo ni kwa sababu anaingia chini ya usimamizi wa muislamu mwanaume. Hii ni fursa kwake kuweza kusilimu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 86-87
  • Imechapishwa: 26/09/2018