Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Daraja ya pili – Bi maana ngazi za dini.

Imani – Imani kilugha ni “kusadikisha”. Kishari´ah ni “kuamini ndani ya moyo, kutamka kwa ulimi na kutenda kwa viungo vya mwili”. Imegawanyika zaidi ya tanzu sabini.

MAELEZO

Zaidi – Ni idadi kutoka tatu mpaka tisa.

Sehemu – Ni sehemu ya kitu.

Kuondosha kitu chenye kudhuru katika njia – Bi maana kuondosha kitu chenye kudhuru ambacho kinawadhuru wapitanjia. Kwa mfano mawe, miba, uchafu, taka, vitu vyenye harufu mbaya na mfano wa hayo.

Hayaa – Ni sifa ya kihemko ambayo inatokea wakati wa mtu anaona aibu na kunamzuia mtu na kufanya kitu ambacho kinaenda kinyume na murua.

Kuoanisha kati ya maneno ya mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) juu ya kwamba imani ni zaidi ya sehemu sabini na kuwa imani nguzo zake ni sita ni ifuatavyo:

Imani ambayo ni ´Aqiydah misingi yake ni sita na ndio ile iliyotajwa katika Hadiyth ya Jibriyl (´alayhis-Swalaatu was-Salaam) wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipomuuliza juu yake. Ndipo akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Imani ni kumuamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Mitume Wake na siku ya Mwisho na  kuamini Qadar kheri na shari yake.”

Kuhusu imani ambayo imekusanya ndani yake matendo, aina na sampuli zake, ni zaidi ya sehemu sabini. Kwa ajili hii ndio maana Allaah ameiita swalah kuwa ni “imani”:

وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُضِيعَ إِيمَانَكُمْ

”Allaah hakuwa Mwenye kupoteza imani zenu.” (al-Baqarah 02 : 143)

Wafasiri wa Qur-aan wamefasiri “imani zenu” kwamba ni zile “swalah zenu mlizoswali kuelekea Yerusalemu”. Kwa sababu Maswahabah kabla ya kuamrishwa kuelekea Ka´bah, walikuwa wakiswali kwa kuelekea Yerusalemu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 79-80
  • Imechapishwa: 31/05/2020