58. Dalili juu ya mkono wa Allaah 19

58- al-Qaadhwiy al-Husayn bin Ismaa´iyl ametuhadithia: Muhammad bin Ishaaq ametuhadithia: Muhammad bin Saabiq ametuhadithia: Ibn Abiy Zaa-idah ametuhadithia: Yahyaa bin Sa´iyd amenihadithia, kutoka kwa Sa´iyd bin Yasaar, kutoka kwa Abu Hurayrah, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyesema:

 “Hakuna yeyote anayetoa swadaqah kutoka katika chumo zuri – na Allaah hakubali isipokuwa kilcho kizuri – isipokuwa anaiweka katika kitanga cha Mwingi wa huruma (Tabaarak wa Ta´ala). Allaah anailea tende hiyo kwa ajili yake, kama anavyolea mmoja wenu mtoto wa ng´ombe, mpaka inakuwa kama Uhud.”[1]

[1] Muslim (1014), an-Nasaa’iy (2525), at-Tirmidhiy (661), Ibn Maajah (1842), al-Bayhaqiy katika ”al-Asmaa’ was-Swifaat” (718), Ibn Khuzaymah (78) na al-Aajurriy (320-321).

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Swifaat, uk. 113-114
  • Imechapishwa: 13/04/2018