57. Makatazo ya muislamu kumrithi kafiri


3- Muislamu hamrithi kafiri na kafiri hamrithi muislamu. Kwa sababu Allaah amekata mafungamano baina yao. Hawarithiani waislamu na makafiri. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Muislamu hamrithi kafiri wala kafiri hamrithi muislamu.”

Hadiyth hii iko katika “as-Swahiyh” kutoka kwa Usaamah bin Zayd (Radhiyaa Allaahu ´anh) [1].

Mirathi ya makafiri hurithiwa na wale ndugu zake makafiri. Haitakiwi kurithiwa na wale ndugu zake waislamu. Ukafiri ni moja ya vizuizi vya mirathi kwa mujibu wa wanachuoni.

[1] Ameipokea al-Bukhaariy (6764) na Muslim (1614) kupitia kwa Usaamah bin Zayd (Radhiya Allaahu ´anh).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 86
  • Imechapishwa: 26/09/2018