57. Kuzika kiungo kilichokatwa kutoka kwa mtu


Swali 57: Ni ipi hukumu ya kukata sehemu ya kiungo maalum kilichozidi kutoka kwa mtu kama kukata kidole au kiungo kingine? Je, kiungo hicho kinatupwa pamoja na takataka au vikusanywe na kumlazimisha mtu kukizika katika makaburi ya waislamu[1]?

Jibu: Jambo ni lenye wasaa. Kiungo hicho hakina hukumu ya mtu. Hapana neno kukiweka katika takataka au kukizika ardhini kwa ajili ya kukiheshimisha, hili la pili ndio bora zaidi. Vinginevyo kama tulivotangulia kusema jambo ni lenye wasaa. Si lazima kukiosha wala kukizika. Isipokuwa ikiwa ni kipomoko kilichotimiza miezi minne. Lakini ikiwa kipande cha nyama ambacho hakijapuliziwa roho au kipande kama cha kidole na mfano wake, jambo ni lenye wasaa. Lakini kukizika katika ardhi yenye udongo msafi ndio vizuri na bora zaidi.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/172).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 43
  • Imechapishwa: 25/12/2021