57. Kuswali na kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah ni shirki II

Hivyo mwambie: “Ukimchinjia kiumbe, sawa awe ni Mtume, jini au wengine, je, utakuwa umeshirikisha katika ´Ibaadah hii asiyekuwa Allaah?” Hana budi kukubali na kusema: “Ndio”. Hivyo mwambie: “Washirikina ambao waliteremshiwa Qur-aan, je walikuwa wakiabudu Malaika, watu wema, Laat na wengineo?” Hana budi kusema: “Ndio”. Hivyo mwambie: “Je, kuwaabudu kwao ilikuwa tu ni katika du´aa, kuchinja na kutafuta kinga kwao na mfano wa hayo? Vinginevyo walikuwa wakikiri kuwa ni waja Wake, chini ya uwezo Wake na kwamba Allaah ndiye Mwenye kuyaendesha mambo, lakini waliwaomba na kuwategemea kwa sababu walikuwa na jaha na maombezi – na hili ni jambo liko wazi sana.”

MAELLEZO

Washirikina wa mwanzo shirki zao hazikuwa isipokuwa katika mambo haya. Qur-aan imeteremka kuwakemea na ikaamrisha kuwapiga vita na kuhalalisha mali na damu zao. Hawakuwa wakiitakidi kuwa masanamu yao yanaumba, yanaruzuku, yanahuisha na yanafisha. Hapakuwa sababu nyingine ya kuwaomba isipokuwa ni kwa ajili ya uombezi. Vivyo hivyo waabudu makaburi hii leo wanayaomba makaburi na watu wema na wala hawaitakidi juu yao kuwa wanaumba, wanaruzuku na kwamba wameumba mbingu na ardhi. Wamewachukua ili kuwatatulia matatizo yao na kutawasali kwao kwa Allaah ili wawaombee na wawakurubishe Kwake na kuomba kinga kwao ili wawaondoshee matatizo na majanga.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 85
  • Imechapishwa: 16/01/2017