Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Dalili ya hajj ni maneno Yake (Ta´ala):

وَلِلَّـهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلًا ۚ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ عَنِ الْعَالَمِينَ

”Na kwa ajili ya Allaah ni wajibu kwa watu watekeleze hajj katika Nyumba kwa mwenye uwezo kuiendea. Na atakayekanusha, basi hakika Allaah ni mkwasi kwa walimwengu.” (Aal ´Imraan 03 : 97)

MAELEZO

Dalili inayoonyesha kuwa ni wajibu ni maneno Yake (Ta´ala):

وَلِلَّـهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ

”Na kwa ajili ya Allaah ni wajibu kwa watu watekeleze hajj katika Nyumba… ”

Aayah hii iliteremka mwaka wa tisa baada ya Hijrah na hapo ndipo hajj ilifaradhishwa. Lakini Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلًا

”… kwa mwenye uwezo kuiendea.”

Hapa kuna dalili kuwa yule asiyekuwa na uwezo wa kuitekeleza basi haimuwajibikii.

وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ عَنِ الْعَالَمِينَ

“Na atakayekanusha, basi hakika Allaah ni mkwasi kwa walimwengu.”

Hapa kuna dalili ya kuwa ni kufuru kuacha kuhiji kwa yule mwenye uwezo kufika huko. Hata hivyo ni kufuru isiyomtoa mtu nje ya Uislamu kwa mujibu wa maoni ya jopo la wanachuoni. ´Abdullaah bin Shaqiyq amesema:

“Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuna kitu katika matendo walikuwa wakionelea kukiacha ni kufuru isipokuwa swalah.”[1]

[1] at-Tirmidhiy (2757). al-Albaaniy amesema:

”Swahiyh.” (Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy (3/44))

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 77-78
  • Imechapishwa: 31/05/2020