57. Dalili juu ya mkono wa Allaah 18

57- Abu Muhammad bin Swaa´id amenihadithia: Ya´quub bin Ibraahiym ad-Dawraqiy ametuhadithia: Wakiy´ bin al-Jarraah ametuhadithia: ´Abbaad bin Mansuur ametuhadithia, kutoka kwa al-Qaasim bin Muhammad: Nilimsikia Abu Hurayrah akieleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´´alyhi wa sallam) amesema:

“Allaah (´Azza wa Jall) anakubali swadaqah na anaipokea kwa mkono Wake wa kuume. Halafu anailea kwa ajili ya mmoja wenu, kama ambavyo mmoja wenu anavyomlea mtoto wa ng´ombe, kisha tonge lile linakuwa kama Uhud. Uthibitisho wa hilo uko katika Kitabu cha Allaah (´Azza wa Jall):

أَلَمْ يَعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ هُوَ يَقْبَلُ التَّوْبَةَ عَنْ عِبَادِهِ وَيَأْخُذُ الصَّدَقَاتِ

“Je, hawajui kwamba Allaah ndiye anayepokea tawbah kutoka kwa waja Wake na anapokea swadaqah?”[1]

يَمْحَقُ اللَّـهُ الرِّبَا وَيُرْبِي الصَّدَقَاتِ

”Allaah huifuta baraka ribaa na huzibariki swadaqah.”[2]

Ameipokea al-Bukhaariy katika kitabu cha Tawhiyd.

[1] 09:104

[2] 02:276

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Swifaat, uk. 109-103
  • Imechapishwa: 09/04/2018