56. Uwajibu wa kutulizana katika Sujuud


Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha Rukuu´ na Sujuud vifanywe ipasavyo na akimfananisha yule asiyefanya hivo na mtu anayekula tende moja au mbili; hazimnufaishi kitu. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mtu kama huyo ni miongoni mwa wezi wabaya kabisa.

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amehukumu kubatilika kwa swalah ya ambaye haunyooshi sawasawa mgongo wake katika Rukuu´ na Sujuud, kama ilivyotangulia kutajwa katika mlango unaozungumzia Rukuu´.

Alimwamrisha (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yule mtu aliyeswali kimakosa kutulizana katika Sujuud, kama ilivyotangulia kutajwa katika mlango wa kwanza.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 126
  • Imechapishwa: 04/08/2017