Mwanamke kumpa haki ya kujichagulia mume anayenasibiana naye haina maana kwamba amepewa uongozi wa kuchagua mume anayemtaka japokuwa hilo litakuwa na madhara juu ya ndugu na familia yake. Hilo limefungamana na yule mlezi wake ambaye atamwelekeza katika kuchagua kwake na jambo lake na vilevile atasimamia kumuozesha kwake. Kwa msemo mwingine haifai kwake kujiozesha. Akijiozesha mwenyewe ndoa ni batili. Imepokelewa katika “as-Sunan” kupitia kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ambaye amesimulia:

“Mwanamke yeyote ambaye atajiozesha mwenyewe bila idhini ya walii wake, basi ndoa yake ni batili, ndoa yake ni batili… “

Katika “as-Sunan” za watunzi wanne imekuja:

“Hakuna ndoa isipokuwa kwa walii.”

Hadiyth hizo mbili na zengine zilizokuja zikiwa na maana kama hiyo zimefahamisha kwamba ndoa haisihi isipokuwa kupitia walii. Kwa sababu msingi katika ukanushwaji ni ukanushwaji wa kusihi. Ibn-ul-Mundhir amesema:

“Ndilo wanachuoni wanalolitendea kazi akiwemo ´Umar, ´Aliy, Ibn ´Abbaas, Abu Hurayrah na wengineo. Vivyo hivyo imepokelewa kutoka kwa wanachuoni wa Taabi´uun kwamba wamesema “Hakuna ndoa isipokuwa kwa walii.” Hayo ndio maoni ya ash-Shaafi´iy, Ahmad na Ishaaq.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tanbiyhaat, uk. 105
  • Imechapishwa: 20/11/2019