56. Ni bora kumswalia maiti msikitini au uwanjani?


Swali 56: Ni bora kumswalia maiti msikitini au uwanjani[1]?

Jibu: Uwanjani ndio bora ikiwa kuna wepesi. Vilevile inafaa kumswalia msikitini kama ambavo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimswalia Ibn Baydhwaa´ msikitini. Hayo yamepokelewa na Muslim katika “as-Swahiyh” yake kupitia kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa)[2].

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/164).

[2] Muslim (973).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 41
  • Imechapishwa: 25/12/2021