56. Hatamu ya maadili katika kuamini Qadar

Yule mwenye kupinga moja katika ngazi hizi anakufuru. Amesema (Ta´ala):

مَا أَصَابَ مِن مُّصِيبَةٍ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي أَنفُسِكُمْ إِلَّا فِي كِتَابٍ

“Hausibu msiba wowote katika ardhi au katika nafsi zenu isipokuwa umo katika Kitabu [Chetu]… “

Kitabu kunalengwa Ubao uliohifadhiwa.

مِّن قَبْلِ أَن نَّبْرَأَهَا

“… kabla Hatujauuumba.”

Kabla ya kuuumba. Ni uandishi:

إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ

“Hakika hayo kwa Allaah ni mepesi.”

Allaah ameumba kila kitu, amekadiria kila kitu na ameandika kila kitu – ni mepesi Kwake (Subhaanahu wa Ta´ala). Ni kwa nini Allaah anatueleza haya? Kwa sababu amesema:

لِّكَيْلَا تَأْسَوْا عَلَىٰ مَا فَاتَكُمْ

”… ili msisononeke juu ya yale yaliyokuondokeeni… “

Unapopatwa na kitu na ukajua kuwa kimekadiriwa na Allaah, basi husikitiki wala kuvunjika moyo:

مَا أَصَابَ مِن مُّصِيبَةٍ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي أَنفُسِكُمْ إِلَّا فِي كِتَابٍ مِّن قَبْلِ أَن نَّبْرَأَهَا ۚ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ لِّكَيْلَا تَأْسَوْا عَلَىٰ مَا فَاتَكُمْ وَلَا تَفْرَحُوا بِمَا آتَاكُمْ

“Hausibu msiba wowote katika ardhi au katika nafsi zenu isipokuwa umo katika Kitabu [Chetu] kabla Hatujauuumba. Hakika hayo kwa Allaah ni mepesi. [Mambo ni hivyo] ili msisononeke juu ya yale yaliyokuondokeeni na wala msifurahie kwa yale Aliyokupeni.”[1]

Usifurahi kwa furaha ya kujiona, shari na kiburi.

[1] 57:22-23

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 45
  • Imechapishwa: 03/08/2021