56. Hakuombwi kwa Uso wa Allaah isipokuwa Pepo tu

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

1- Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna kinachoombwa kwa uso wa Allaah isipokuwa Pepo.”[1]

Ameipokea Abu Daawuud.

MAELEZO

1- Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna kinachoombwa kwa uso wa Allaah isipokuwa Pepo.”

Haya kwa sababu Pepo ndio malengo makubwa. Ndani yake utaonekana uso wa Allaah (Subhaanah) na ndani yake kuna neema zisizokatika. Uso wa Allaah ni wenye utukufu mkubwa. Kwa hivyo haifai kuomba kwa uso wa Allaah isipokuwa Pepo.

Vivyo hivyo inahusiana na yale yote yanayopelekea katika Pepo kama vile Ikhlaasw, kuafikishwa juu ya kheri na kunyooka juu ya utiifu. Kila ambacho kinapelekea katika Pepo kinaingia katika kuomba Pepo.

 Haya ni miongoni mwa ukamilifu wa Tawhiyd na imani mtu kutoomba kwa uso wa Allaah isipokuwa Pepo na yale yote yanayopelekea katika Pepo kama vile matendo mema, kunyooka na kusalimika kutokamana na upotevu na mitihani mbalimbali.

Katika cheni ya wapokezi kuna udhaifu, lakini unatiwa nguvu na mapokezi mengine yanayokataza kuomba kwa uso wa Allaah. Kwa njia hiyo Hadiyth hii inakuwa maalum na inajuzisha kuomba kwa uso wa Allaah mtukufu na yale yote yanayopelekea katika Pepo.

[1] Abu Daawuud (368). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwa´iyf Sunan Abiy Daawuud” (368).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kitaab-it-Tawhiyd, uk. 158
  • Imechapishwa: 08/11/2018