Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Dalili ya swawm ni manneo Yake (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ

“Enyi mlioamini! Mmefaradhishiwa swawm kama ilivyofaradhishwa kwa walio kabla yenu mpate kuwa na uchaji Allaah.” (al-Baqarah 02 : 183)

MAELEZO

Dalili ya inayoonyesha kuwa swawm wajibu ni maneno Yake (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ

“Mmefaradhishiwa swawm kama ilivyofaradhishwa kwa walio kabla yenu mpate kuwa na uchaji.”

Katika maneno Yake “kama ilivyofaradhishwa kwa wale walio kabla yenu” kuna faida zifuatazo:

1- Umuhimu wa swawm kwa kule Allaah (´Azza wa Jall) aliifaradhisha kwa nyumati zilizotangulia kabla yetu. Hii inajulisha mapenzi ya Allaah (´Azza wa Jall) juu yake na kwamba ni lazima kwa kila Ummah.

2- Wepesi juu ya Ummah huu. Kwa sababu swawm hawakufaradhishiwa wao wenyewe, jambo ambalo linaweza kuwa na ugumu kwa nafsi na viwiliwili.

3- Kuna ishara juu ya kwamba Allaah (Ta´ala) amekamilisha dini juu ya Ummah huu kwa vile alikamilisha fadhila Zake ambazo wengine walitangulia kuwa nazo.

Mpate kuwa na uchaji Allaah – Allaah (´Azza wa Jall) amebainisha katika Aayah hii hekima ya swawm kwa kusema:

لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ

“… mpate kuwa na uchaji Allaah.”

Maana yake ni kwamba ili mumche Allaah kwa funga zenu na yanayopelekea katika kufikia uchaji Allaah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameashiria faida hii pale aliposema:

“Asiyeacha maneno ya uongo na kuyafanyia kazi, basi Allaah hana haja kwa yeye kuacha chakula na kinywaji chake.”[1]

[1] al-Bukhaariy (1903) na (6057), Abu Daawuud (2362), at-Tirmidhiy (707), Ibn Maajah (1689) na Ahmad (2/354).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 77
  • Imechapishwa: 31/05/2020