31. Dalili ya kumi na nane kutoka katika Sunnah juu ya mikono ya Allaah

32- Jaabir al-Answaariy (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Pindi Allaah alipomuumba Aadam na kizazi chake Malaika walisema: “Ee Mola! Umewaumba watu na kuwafanya ni wenye kula, wenye kunywa na ni wenye kuoa. Wajaalie dunia na sisi Aakhirah.” Ndipo Allaah (´Azza wa Jall) akasema: “Sintojaalia ambaye nimemuumba kwa mkono Wangu na nikampulizia sehemu ya roho Yangu kama kile nilichosema “Kuwa!” na kikawa.”[1]

[1] al-Bayhaqiy katika ”al-Asmaa’ was-Swifaat” (688). adh-Dhahabiy amesema:

”Cheni yake imesalimika.” (al-´Uluww, uk. 66)

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaat-ul-Yad li-Laah Swifatan min Swifwaatih, uk. 28
  • Imechapishwa: 02/07/2019